December 2, 2020




SELEMAN Matola, Kocha Msaidi wa Klabu ya Simba anatajwa kuingia anga za Azam FC ambao wanasaka mbadala wa Aristica Cioaba


Cioaba alifutwa kazi Novemba 26 ikiwa ni siku moja baada ya timu ya Azam FC kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Yanga, mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Azam Complex. 


Kwa sasa Azam FC ipo chini ya Kocha Msaidizi, Vivier Bahati na mchezo wake wa Kwanza alilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Biashara United Uwanja wa Karume.


Cioaba kabla ya kufutwa kazi alipoteza mechi mbili mfululizo alianza kufungwa bao 1-0 dhidi ya KMC kisha akapoteza mbele ya Yanga jambo lililowafanya mabosi wake kumfungia virago.


Habari zinaeleza kuwa kabla ya kuongeza mkataba ndani ya Azam FC, Matola alikuwa kwenye mazungumzo na Azam FC ila dili lake lilibuma kutokana na mwendo ambao alianza nao raia huyo wa Romania.


Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa kwa sasa majina mengi yanatajwa hivyo mashabiki wasiwe na mashaka kila kitu kitakuwa sasa.


"Kuna majina mengi kweli kwa sasa yanatajwa ila hakuna tatizo kwa sababu Azam FC ni timu kubwa, mchakato unaendelea na baada ya muda kila kitu kitakuwa sawa," amesema.

9 COMMENTS:

  1. Hopeless kabisa...Kwan una haraka gani ya kuandika? Huwezi hata kuhariri ulichoandika? Kichwa cha habari kinataja Yanga, habari yenyewe inataja Azam..Badilikeni basiiii, amaaaaa

    ReplyDelete
  2. Saleh jembe yaani sasa bora fungeni blog hii maana hata hamjui mnacho andika au umeme ulikatika ni aibu kubwa sana unaweza kushtakiwa

    ReplyDelete
  3. sababu habari zenyewe wanajitungia tu... ndo Maana wanakosa Kabisa umakini

    ReplyDelete
  4. Hahahaha hawa wandishi wanaandikia kwenye mwanga wa kibatari

    ReplyDelete
  5. Hey there, I’m John. I’m a software engineer living in City Centre, Sunderland SR1 3AP, UK.You can visit my company website with a click on the button above.
    Mcafee.com/activate
    Norton.com/setup
    Office.com/setup
    Mcafee.com/activate
    Webroot.com/safe



    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic