December 7, 2020


 SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba, amewataka wachezaji wake kucheza kwa tahadhari katika kusaka matokeo ndani ya uwanja kwani wana kibarua cha kukusanya pointi tatu kwenye kila mechi za Ligi Kuu Bara.

 

Raia huyo wa Ubelgiji amesema kuwa, wanapaswa kucheza kwa umakini kusaka matokeo huku wakichukua tahadhari kwa sababu ya mechi zingine zilizo mbele yao.

 

“Baada ya mechi dhidi ya Plateau United, katikati ya wiki tutakuwa na mechi, sasa hapo kwa namna yoyote ni lazima wachezaji wacheze kwa tahadhari.

 

“Lengo kwenye mechi zetu za ligi ni kuendeleza kasi ile ambayo tuliishia kwenye mchezo wa mwisho ili kupunguza pointi ambazo tumezidiwa na wapinzani wetu.

 

“Tunatambua kwamba tuna kazi ya kutetea ubingwa, hilo halitawezekana ikiwa tutashindwa kupata ushindi,” amesema Sven.


 Katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, Simba ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 23 baada ya kucheza mechi 11. Yanga inaongoza ligi ikikusanya pointi 34 baada ya kucheza mechi 14.


Mchezo unaofuata kwa Simba ni dhidi ya Polisi Tanzania utakaochezwa Desemba 9, Uwanja wa Mkapa.

2 COMMENTS:

  1. Kocha ana point. Yanga watajaribu kila aina ya uchafu kucheza na viporo vya simba ni vizuri kuwa makini kunako kila idara.

    ReplyDelete
    Replies
    1. YANGA WANASAIDIWA NA WATU WASIOJULIKANA NDIYO MAANA KILA UCHWAO LAZIMA WASEPE KWA MKONO WA MTU

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic