KIKOSI cha Gwambina FC leo Desemba 7 kimegawana pointi mojamoja na Azam FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Gwambina Complex.
Nahodha wa kikosi cha Gwambina FC, Jacob Masawe amesema kuwa haukuwa mpango wao kupata sare kwenye mchezo wa leo kwa kuwa walijipanga vema kupata ushindi ili wasepe na pointi tatu jumlajumla.
Gwambina walionekana kuwa bora kipindi cha pili ambapo walishambulia lango la Azam FC lililowekwa salama na kipa namba mbili Benedict Haule.
Masawe alikosa nafasi mbili za wazi katika harakati za kusaka ushindi kwa timu yake jambo ambalo lilimfanya ashike kichwa mara kwa mara.
Kwa upande wa Azam FC, nyota wao Ayoub Lyanga amesema kuwa ni matokeo kama yalivyo matokeo mengine ndani ya uwanja na hawakuwa na chaguo kwa kuwa walipambana.
Azam ilikosa pia nafasi za kufunga katika kipindi cha pili na kuwafanya wafikishe pointi 27 wakiwa nafasi ya pili baada ya kucheza jumla ya mechi 14.
Gwambina FC wao wanafikisha jumla ya pointi 17 wakiwa nafasi ya 10 baada ya kucheza mechi 10 ndani ya Ligi Kuu Bara.
Kwa jinsi hiyo ubingwa basi tena.
ReplyDeleteUbingwa ndo basiii tenaaa kwa azam!!
ReplyDeleteAzam vibonde tu hao mpka mwisho wa ligi wanaweza kujikuta nafasi ya 5
ReplyDeleteSi kweli Azam baado ananafasi
ReplyDeleteHakuna cha nafasi yanga Na simba safari hii zinamaanisha.
DeleteDah! Azam ndo Basi tena, wasubiri mbeleko za Simba tunakwenda kuongeza team kimataifa safari hii
ReplyDelete