JONATHAN Nahimana kipa namba moja wa Klabu ya Namungo FC anatajwa kuingia kwenye rada za mabosi wa Simba ili akamuongezee changamoto kipa namba moja Aishi Manula.
Habari zinaeleza kuwa raia huyo wa Burundi zama zile alipokuwa ndani ya KMC ilibaki kidogo ajiunge na Simba kwa kuwa alikuwa anamvutia Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck ila uwepo wa kipa Beno Kakolanya ulifanya nyota huyo asiweze kupata nafasi ndani ya kikosi hicho.
Nahimana ambaye ni raia wa Burundi aliweka wazi kwamba miongoni mwa timu ambazo zilikuwa zinahitaji saini yake ni pamoja na Simba hivyo kwa sasa anasubiri kuona nini kitatokea.
"Msimu uliopita Simba walinifuata mara mbili wakihitaji kupata saini yangu ila kuna mambo yalikwama kwa sasa bado sijafuatwa hivyo ni jambo la kusubiri.
"Mbali ya Simba pia hata Yanga nao pia walinifuata ambapo walikuwa wanahitaji kunisajili mwisho wa siku mambo yalikwenda tofauti.
"Kwa sasa nipo ndani ya Namungo nitapambana kimataifa ili kufika mbali nina amini kwamba sitaweza kukosa timu," amesema.
Simba ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 32 baada ya kucheza mechi 14, imefungwa mabao matano ambapo manne amefungwa Manula na moja alifungwa Kakolanya.
Nahimana kwa sasa yupo Namungo ambapo amepelekwa kwa mkopo akitokea Klabu ya KMC.
Acheni uongo, kisa mmeona jana beno alikosea kidogo leo mnataka kuuza habar za uongo
ReplyDeleteKakolanya ni bora sana kuliko huyo unayempigia promo
ReplyDelete