December 20, 2020

 


LEICESTER City imesepa jumla na pointi tatu zote mbele ya Tottenham Hotspur kwa ushindi wa mabao 2-0.


Ikiwa ugenini, Leicester City ilianza kupachika bao la kwanza dakika ya 45+4 kwa mkwaju wa penalti iliyofungwa na Jamie Vardy.


Kipindi cha pili ndani ya Uwanja wa Tottenham Hotspur dakika ya 59, Toby Alderweireld alijifunga bao la pili na kuongeza mzigo kwa kikosi hicho cha Jose Mourinho. 


Mpaka dakika 90 zinakamilika Spurs wameshuhudia pointi zikisepa jumla na kuwaacha na 25 wakiwa nafasi ya 5 na pointi 25.


Leicester City inajijengea ufalme nafasi ya pili ikiwa na jumla ya pointi 27 zote zimecheza jumla ya mechi 14.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic