December 21, 2020

2 COMMENTS:

  1. Kueleza kwa kifupi ukweli bila ya ushabiki wazungu wanasema unbiased facts kuhusiana na kikosi cha simba na ubora wake na nini cha kufanya ili kuepuka setback ama kushindwa kuja kufikia malengo waliojiwekea.
    Tukianzia kwenye benchi la ufundi. Kocha na wasaidizi wake kwa sasa wapo sawa. Sven ni kocha anaejiamini na ni jambo muhinu sana kwa kocha kama kiongozi kwani kujiamini kwake ndiko kunakowajenga wachezaji wake kujiamini hata kama atakuwa anamapungufu yake ndio uninaadamu. Ukiangalia tangu simba wamfukuze kocha wa makipa kiwango cha Manula kimepanda sijui kuna siri gani? Kuhusu kikosi.Simba ina wachezaji wengi wazoefu ila kuna baadhi ya wachezaji simba kama vile mvuvi mahiri alieridhika kuishia kuvua samaki ufukweni peke yake wakati uwezo anao wa kwenda maji makubwa na kuongeza kipato chake hadi kumtajirisha zaidi.sasa sijui ni uoga,uvivu au uzembe? Au pengine kukosa walimu bora wa akili.Ila suala la kujiamini ni moja ya tatizo kubwa linalotumaliza watanzania kushindwa kufanya vizuri kwenye maeneo yetu mbali mbali ya kazi. Tiliona juzi waziri mtaalamu mbobezi lakini alishindwa kula kiapo mbele ya Raisi. Nnachotaka kusema kuwa kuna wachezaji simba wana uwezo mkubwa na uzoefu pia lakini wanashindwa kujiamini na kuishia kuozea benchi.Tatizo la mtu au mchezaji kukosa kujiamini linasababishwa na mambo mengi. Kwanza kabisa ni ukosefu wa maandalizi au maandilizi duni ya mtu husika au mchezaji kabla ya kazi husika.Mchezo wa mpira ni mchezo wa akili na kimwili na ni mchezo wa hadharani kwa hivyo aliejiandaa vyema ndie aliejiandalia ushindi uwe ushindi wa namba kwa mchezaji kupata kucheza au hata kwa timu nzima kupata ushindi.Kiuhalisia labda mchezaji awe anasumbuliwa na majeraha ila kwa mchezaji ukiona umesajiliwa na timu kama simba basi walishakuona kuwa kuna kitu na ukiendelelea kukubali kukaa benchi sio kosa la kocha ni wewe mwenyewe utizame wapi unakosea ujirekebishe hata kocha kama hakupangi basi timu nyengine zenye kaliba ya simba ziwe zinakuhitaji. Kwa uongozi wa simba wanatakiwa kuwa makini sasa au watafeli vibaya msimu huu.Ukiangalia Yanga walifanya usajili mzuri kuliko simba Dirisha kubwa huo ndio ukweli na mpaka sasa ameshafanya usjili bora zaidi kwenye Dirisha dogo kwa saido huo ndio ukweli. Ukweli ni kwamba simba inakosa mshambuliaji mwenye afya mwenye uwezo wa kupambana na mabeki na vile vile wanahitaji kiungo mchezeshaji mwenye malengo zaidi ya upambanaji kuja kumfanya chama awe huru zaidi.Hapa kocha atalaumiwa bure kama uongozi hautorekebisha makosa ya usajili uliofanyika Dirisha kubwa. kuhusu backline ya simba hivi sasa kwa kweli inaonekana ipo very stable.Simba itaepuka gharama ya kusajili wachezaji wapya kama tu wachezaji wake wa sasa wataamua kuamka na kutambua uwezo na kupambana kwa ajili ya timu yao kwani ni moja ya timu inayowatunza wachezaji wao vyema na wachezaji nao lazima wawe na shukrani kwa timu yao katika kuipigania uwanjani. Lakini kwa ninavyiona simba ya sasa wanahitaji mshambuliaji wa kuamua mechi tena haraka. Tunawatakia simba ushindi Zimbabwe hakuna kisicho wezekana ni kupambana mwanzo mwisho. Hii mechi ni fainali na ni kwa wachezaji wenywewe kukaa chini na kukabidhiana majukumu sio suala mchezaji kusubiri kocha amwambie nini cha kufanya. Kusonga mbele simba ndio kuongezeka kwa ubora wa mchezaji mmoja mmoja. Wachezaji wa Platinum wataingia uwanjani wakiwa na malengo makuu matatu(1)Kucheza kwa bidii ili kuonekana na viongozi wa simba kwanza katika kutafuta kandarasi ndani ya simba.(2) kutimiza majukumu ya timu yao kuhakikisha wanaingia hatua ya makundi.(3)Kulinda heshima ya taifa lao yaani uzalendo zaidi na kujitangaza zaidi. Tunaimani wachezaji wa simba wana uwezo wa kuwakaibili platinum na kupata matokeo mazuri.

    ReplyDelete
  2. Mimi naomba nijiongeze kwa kifupi ,hii Blog inamilikiwa na mtu binafsi na ni ukweli,Lkn Mr hapa don't play mind game kwa kutanguliza ur personal interest na Kambi Fulani ku fool watu ,mimi nimekuwa mshiriki kwenye haya Lkn na realize ukweli na kuelewa deals zenu ,hamtakiwi kuaminiwa na Jamii ,kwa maaana brother kwenye hili, naomba nikuulize Gazeti la Champion Pg 14&15 hapa Mr Makumbi then the following page Saidio ,huku mtu wa kwanza anaonekana anataabika lkn aliitumikia Yanga japo alifurahia maisha Yanga,.Hapa naomba niwaongoze mnaosoma makala au Taarifa yoyote bila kujua mantiki au dhumuni la Mwandishi,Mkuu kwa kifupi iache Yanga iitwe
    Yanga ,Mimi nimekuwa nakunukuhu mala nyingi ,makala au Takwimu Kama hizi za Saidio ulizotoa,tungezipata kwa Bwalya ,Mugalu ningekuelewa bt you keep on briefing and analazying once a player wa Caribre ya Morrison performs akiwa Yanga halafu akasifiwa ,bt then after utasikia mkataba then mtaanza kutuandikia hapa ndipo walipo kosea Yanga (Morrison). kinachofata ni upuuzi mtupu,najua hii ni Biashara bt kuwa ukweli pande zote Linda professional yako haswa,Mambo ya Friends of Simba achana nayo,habari za kutunga hili uwa demolize Mastriker wa Yanga kwa hii Yanga in general yanashusha thamani ya Gazeti lako unapotezewa tu na kivuli Cha Gazeti .Tuisenge and co una wa uchuuza Wananchi ,bt hawachuuziki.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic