December 6, 2020

 


FT: Yanga 2-1 Ruvu Shooting 
Uwanja wa Mkapa

Yanga imesepa na pointi tatu mbele ya Ruvu Shooting kwa ushindi wa mabao 2-1 na kufikisha jumla ya pointi 34.

Inajikita kileleni ikicheza jumla ya mechi 14 bila kupoteza kwa msimu wa 2020/21.

Dakika 3 zinaongezwa 
Dakika 90 Dabi anapeleka mashambulizi kwa Yanga
Dakika ya 78 Yanga wanapiga kona ya 8 Ruvu ikiwa imepiga kona 1
Dakika ya 75 Niyonzima anapiga faulo inadakwa na Abdallah Rashid
Dakika ya 71 Niyonzima ndani anatoka Kaseke
Dakika ya 65 Cassian Mponela Goaaal la kujifunga kwa Ruvu Shooting 
Dakika ya 59 Gooooal David Richard baada ya kosa la Lamine Moro kutoa pasi ndani ya 18
Dakika ya 58 anakosa penalti 
Dakika ya 57 Kaseke anapewa jukumu la kupiga penalti, baada ya mwamuzi kuamua ipigwe kwa kutafsiri Reantus
Dakika ya 56 Yanga wanapata penalti
Dakika ya 50, Renatus anaonyeshwa kadi ya njano
Dakika ya 49 Kisinda anachezewa faulo
Dakika ya 47 Kaseke anachezewa faulo na dabi
Dakika ya 46 Dabi anazuia mashambulizi 
Kipindi cha pili kimeanza 
KIPINDI cha kwanza, Mapumziko 

Uwanja wa Mkapa 

Ligi Kuu Bara 

Desemba 6


Yanga 1-0 Ruvu Shooting


Zinaongezwa dk 2

Dakika ya 45 Kaseke anacheza faulo inapigwa na Abdulrahman Mussa haizai matunda 

Dakika ya 41 Kibwana Shomari anaonyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea faulo Abdulhaman Mussa

Dakika ya 36 Yanga wanapeleka mashambulizi kwa Ruvu

Dakika ya 30 Sarpong anafunga Gooool ndani ya 18

Dakika ya 28 Sarpong anachezewa faulo

Dakika ya 23, Mnata anaokoa hatari ndani ya 18 kwa mguu

Dakika ya 21 Ruvu Shooting wanapeleka mashambulizi kwa Mnata 

Dakika ya 18 Kisinda anafanya jaribio linakwenda nje kidogo ya lango

Dakika ya 14 Mustapha anapiga faulo haizai matunda inagonga ukuta wa Ruvu Shooting 

Dakika ya 12 Nyosso anaonyeshwa kadi ya njano

Dakika ya 10 Kaseke anapiga faulo haizai matunda 

Dakika ya 8 Banka anapewa huduma ya kwanza 

Dakika ya 6 Kaseke anapiga kona ya Kwanza kwa Yanga haizai matunda 

Dakika ya 02 Mustapha anapewa huduma ya kwanza


Februari 8 mchezo wa mwisho msimu uliopita, Yanga ilishinda bao 1-0 lilifungwa na David Molinga

11 COMMENTS:

  1. Mukoko Tonombe amemkanyaga banka kichwani kwa makusudi.... Anastahidi adhabu

    ReplyDelete
  2. Walifanya wenzenu ohh wanabebwa.

    ReplyDelete
  3. Replies
    1. Ndo unaona mkwasa na yanga baada ya kuongeza la pili?
      Ksma kuna tabia za kikez

      Delete
    2. Ilikuwa moja bila hutazami muda msg ilipoandikwa?Na magoli yalivyofungwa?

      Delete
  4. Kwani mpira siku hizi unachezwa kwa mikono maana kaseke goli la kwanza kaukumbatia mpira kama Rede alafu Refa anajifanya hajaona. Toka ligi ianze sijaona Yanga akicheza mechi bila kuwa na Goli la utata. Halafu magoli ya timu pinzani yanakatakliwa hamna timu hapo ni utopolo mtupu

    ReplyDelete
  5. Masau kaongea bonge la point,, ndani ya ruvu yumo yuda ndo aliyesababisha kufungwa kwao. Nahic mkwasa ndo jipu kuwabeba utopolo wenzie .

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mtu akifa yanaongelewa mambo mengi sana. Hata timu ikifungwa vijisababu vya kujitetea havikosagi

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic