December 6, 2020


 MTENDAJI Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin amesema kuwa sababu kubwa ya kumshusha George Lwandamina ni kutokana na rekodi zake kitaifa na kimataifa jambo ambalo wanaamini atafanya vizuri.


Azam FC ambayo ilianza kwa kasi msimu wa 2020/21 ilishinda mechi saba mfululizo na kukusanya pointi 21 huku ikiwa nafasi ya kwanza kabla ya kushushwa na Yanga, kasi yake ilipungua ghafla na kwenye mechi sita za hivi karibuni ilivuna pointi tano.


Ilimfuta kazi Aristca Cioaba, Novemba 26 siku moja baada ya kufungwa bao 1-0 na Yanga Uwanja wa Azam Complex na mikoba yake imechukuliwa na George Lwandamina.


Lwandamina ambaye aliwahi kuifundisha Klabu ya Yanga msimu wa 2016 na aliweza kuipa ubingwa wa ligi, alisepa ndani ya Bongo na kuibukia Klabu yake ya zamani ya Zesco United ya Zambia ila kwa sasa yupo ndani ya Bongo tena.


Akizungumza na Saleh Jembe, Amin amesema kuwa wana matumaini makubwa kwa Lwandamina kutokana na uzoefu wake.


"Tunatarajia kukaa naye kwa muda wa msimu mmoja kwenye viunga vya Azam FC ila kwa namna atakavyofanya kazi basi tutazidi kushirikiana naye.


"Uzoefu wake kwa kufundisha soka la Afrika ni sababu ya sisi kuhitaji huduma yake hivyo tunaamini kwamba tutakwenda naye sawa , mashabiki wazidi kutupa sapoti tuna amini tatafanya vizuri," amesema.


Kwa sasa Azam FC ipo mkoani Mwanza ambapo kesho Desemba 7 itakuwa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Gwambina FC, utakaochezwa Uwanja wa Gwambina Complex kikiwa pamoja na Lwandamina ambaye amesaini dili la mwaka mmoja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic