December 28, 2020



NYOTA wanne wa Klabu ya KMC wana Kino Boys ambao walikuwa wanasumbuliwa na majeraha wamerejea kazini kwa ajili ya kuanza kazi kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City. 

 Abdul Hillary, Hassan Kapalata hawa walikuwa wakisumbuliwa na majeraha mbalimbali ya muda mrefu, wamerejea rasmi leo Desemba 27 kuungana na wachezaji wenzao kwenye mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa mzunguko wa pili.


Kapalata na Hillary hawakuwa pamoja na timu kwa muda wa mwezi mmoja kutokana na kusumbuliwa na majeraha.


Wengine waliokuwa wanaumwa na kurejea kwenye mazoezi ni pamoja na Hassan Kabunda ambaye aliumia katika mchezo dhidi ya Simba na hivyo kushindwa kucheza katika michezo miwili ambayo ni dhidi ya Ihefu pamoja na JKT Tanzania.


Mchezaji mwingine ambaye ameungana na wenzake katika mazoezi ya leo ni pamoja na David Brayson ambaye alikuwa kwenye Timu ya Taifa ya Vijana Ngorongoro Heroes.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic