PETER Tarimo ambaye ni shabiki wa Simba na Fatuma Juma shabiki kindakindaki wa Yanga, wamekuwa washindi wa kwanza wa Chemsha Bongo ya Spoti Xtra na kukabidhiwa zawadi zao leo Jumamosi kwenye ofisi za gazeti hilo zilizopo Sinza Mori, Dar.
Chemsha Bongo hiyo iliyoanza wiki iliyopita, inatoa nafasi kwa msomaji wa Gazeti la Spoti Xtra kujishindia zawadi mbalimbali kwa kujibu kwa ufasaha maswali yanayoulizwa katika ukurasa wa pili. Zaidi ya washindi 100 wanatarajiwa kupatikana kupitia Chemsha Bongo hiyo.
Spoti Xtra kwa kushirikiana na Vunjabei Mobile Shop, wauzaji wa vyombo bora vya ndani hapa nchini, wanatoa zawadi hizo ikiwemo friji, microwave, rice cooker, brenda, jiko la gesi, dinner set na nyingine nyingi.
Akizungumza na Spoti Xtra, Tarimo mkazi wa Vingunguti jijini Dar aliyejishindia Brenda, alisema: “Nashukuru kwa kubahatika kushinda zawadi hii, mimi ni shabiki wa Simba na msomaji mkubwa wa Spoti Xtra, nawashauri wengine nao kununua magazeti haya na kushiriki ili washinde. Zawadi zipo nyingi na zinatolewa bila ya upendelezo wowote.”
Naye Fatuma aliyejishindia rice cooker, alisema: “Nalipenda Gazeti la Spoti Xtra kutokana na habari nyingi za Kibongo na kimataifa zilizoandikwa kwa viwango vya hali ya juu, mimi ni shabiki wa Yanga, nawashauri Wanayanga wenzangu pamoja na watani zetu Simba washiriki kwa kununua Spoti Xtra na kushiriki Chemsha Bongo hii, naamini watanishukuru.”
Meneja Masoko wa Kampuni ya Vunjabei Mobile Shop ambaye alikabidhi zawadi hizo kwa washindi, Catherine Peter, alisema: “Napenda kutoa wito kwa wasomaji wa magazeti kuhakikisha wananunua Spoti Xtra ili kujitengenezea nafasi kubwa ya kujishindia zawadi kemkem tunazozitoa wanaposhiriki Chemsha Bongo iliyopo ndani ya gazeti hilo.”
Mhariri wa Gazeti la Spoti Xtra, Omary Mdose, naye alisema: “Kama mnavyofahamu, Spoti Xtra ni gazeti linaloongoza hapa nchini kwa ufanisi wa habari zinazoandikwa zikiwa na takwimu nyingi zilizochambuliwa kwa ufasaha.
“Hivyo usipange kukosa nakala yako, kwani kwa kufanya hivyo unajiweka katika nafasi nzuri ya kushinda zawadi kupitia Chemsha Bongo yetu hii.
“Kwa sasa Spoti Xtra linatoka mara tatu kwa wiki, JUMANNE, ALHAMISI na JUMAPILI, hivyo ukijipatia nakala yako kwa Sh 500 tu, una nafasi kubwa ya kushinda zawadi hizi.”
hivi saleh jembe ndiyo mnajifanya hamjui kwamba kuna habari ya Simba amefuzu kuingia hatua ya pili? mnazingua
ReplyDeleteukiona unachukia wakati mwenzako anafanikiwa..jua wewe una roho ya kichawi
ReplyDelete