December 6, 2020


 BAADA ya Simba  kupenya hatua ya awali na kutinga hatua ya mtoano sasa inaingia mikononi wa Wazimbabwe kwenye hatua ya mtoano.


Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck jana Desemba 5 ililazimisha sare ya bila kufungana na Klabu ya Plateau United kutoka Nigeria Uwanja wa Mkapa.


Inapenya hatua ya mtoano kwa kuwa mchezo wa kwanza wa awali wa  Ligi ya Mabingwa uliochezwa Uwanja wa New Jos Nigeria Simba ilishinda bao 1-0 lililopachikwa kimiani na Clatous Chama.


Mchezo wa kwanza unatarajiwa kuchezwa kati ya Desemba 22-23 nchini Zimbabwe Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe na ule wa marudio unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa kati ya Januari 5-6.

7 COMMENTS:

  1. Hapo kazi ipo tena kubwa lkn kwenye umoja na nia tunaweza kuingia makundi tena.ila umakin unahitajika maana hao jamaa inaonyesha wapo vizuri hasa eneo la ushambuliaji maana wamevuka kwa goli 4-1 wameshinda nje ndan na Tim ya msumbiji

    ReplyDelete
  2. Kwa kuwatupia jicho la mwewe wachezaji wazawa wa simba wanarejea makosa yale yale walioyafanya kwenye champion league zilizopita za kucheza mpira kimazoea na kushindwa kujua kuwa huu ndio wakati wa Do or die katika kujiongeza kwenye viwango vya upambanaji ili ikiwezekana kupata ajira yenye maslahi zaidi. Umemuona Luis Miquisone kwenye mechi na Plateau alivyoipigania simba utadhani amezaliwa ndani ya Simba. Louis Maquisone anajua anachokifanya kwani anajua kupitia mashindano haya ya klabu bingwa Africa ndio yaliomtoa na ndio yatakayomtoa zaidi.Ulimuona Morrison na dakika zake chake alivyowatetemesha wanaigeria wachezaji wazawa wanafeli wapi? Ukiachana Manula,Shabalala,Kapombe na sasa ameongezeka Erasto Nyoni ambao viwango vyao kusema kweli ni vya kimataifa. Mkude ni mchezaji mzuri sana ila ni mchezaji ambae hatabiriki kwenye kutunza kiwango chake kuwa bora muda wote.Muzamiru na khasan Dilunga kwa kiroho safi kabisa ni wachezaji wazuri ila wanakosa uimara wa mwili kwa maana ya pumzi na utimamu wa mwil kutokana na nafasi zao za majukumu uwanjani.Mchezaji wa kiungo halisi tunasema ni mtu mwenye mapafu ya farasi.Ili machezaji wa kiungo wa Caf aweze kuwa na caf champion league ya mafanikio lazima ajitoe kwa mazoezi ya ziada na kujitambua kuwa huu ni wakati wa kuonesha tofauti. Anapofanya mazoezi afikirie kuwa anakwenda kushindana na wachezaji mahiri wa vilabu bora Africa hivyo lazima kujipanga katika utimamu wa mwili mambo ya kiufundi simba ina makocha bora kabisa Africa.
    Ndemla,Ame,na wazawa wengine pale simba wajipange kwa vitendo siku wakipata nafasi kuiwakilisha timu Africa wawe kamili gado na wamshawishi kocha kuwa anafanya makosa kuwaeka benchi.Platinum ni timu nzuri ina wachezaji wanapambana kuonekana kimataifa .kwa hivyo inawachezaji wanaojituma sana simba wawe makini.

    ReplyDelete
  3. Umeandika notes nyingi za somo gani

    ReplyDelete
  4. Platinum out! Simba huu Ni mwaka wetu wengine watasubiri sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Simba unatakiwa kubadilika Sana hasa inapocheza nyumbani,mfumo WA kutumia mshambuliaji mmoja ukiwa home tunashindwa kupata matokeo,wachezaji wasawa kujituma bado baadhi Yao hawajapata kasi Dilunga,Mzamiru Na Mkude utadhani wanacheza ligi,Boko Ni nzuri anakuja kusaidia timu inaposhambuliwa ila hajawa Na kasi ya kutosha kupanda tunaposhambulia,kilamtu akijituma kwa 100% tutafika,Platinum sio wabaya msimu uliopita waliwatoa UD Songo kwa kishindo Na mwaka huu wameingia tena kwa kishindo

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic