UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho Desemba 7 dhidi ya Gwambina FC utakaochezwa Uwanja wa Gwambina Complex.
Mchezo huo utakuwa ni wa 14 kwa Azam FC ambayo ilimfuta kazi Aristica Cioaba raia wa Romania kutokana na mwendo mbovu wa timu hiyo.
Kwa sasa mrithi wa mikoba ya Cioaba ni George Lwandamina raia wa Zambia ambaye amesaini dili la mwaka mmoja.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na wanaamini kwamba watapata ushindi kwenye mchezo huo.
"Tumetoka kulazimisha sare mbele ya Biashara United, tayari mwalimu ameona makosa ya wachezaji na pale ambapo wamekosea hivyo tumejipanga.
"Kwa mazoezi ambayo tumeyafanya hatuna mashaka na nafasi yetu kwenye mchezo hasa ukizingatia kwamba wapo mashabiki wetu wanaotupa sapoti.
"Tutapambana kufanya vizuri ili kurejesha furaha ambayo imekosekana kwa muda, mashabiki watupe sapoti," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment