MENEJA wa nyota wa Plateau United, Isah Ndala amesema kuwa mchezaji huyo ana ofa nyingi kutoka timu mbalimbali ambazo zinahitaji kupata saini yake ikiwa ni pamoja na Yanga.
Ibrahim Ahmed ambaye ni meneja amesema kuwa mchezaji wake amekuwa akiwaniwa na timu nyingi kutokana na uwezo wake ndani ya uwanja.
Miongoni mwa timu ambazo zinatajwa kuwania saini yake ni pamoja na Yanga ambao walivutiwa na uwezo wake baada ya kucheza na Simba kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali.
Ahmed amesema:"Zipo timu nyingi ambazo zinaiwania saini ya mchezaji Ndala kwa sababu ana uwezo mkubwa na anajiamini hivyo nina amini kwamba ikiwa kuna timu itapata saini yake basi itapata faida kubwa.
"Kwa Tanzania zipo timu ambazo tumeanza mazungumzo nazo ikiwa ni pamoja na Yanga ila siwezi kusema kwamba kwa sasa tumefikia wapi na nini kiandelea kwa kuwa ni siri," .
Mbwembwe zimeanza kazi ipo hapo
ReplyDeleteKweli hizi ni mbwembwe tuu. Labda wawape kama zawadi ya kuwapokea na kuwasaidia walipokuja kucheza na simba, vinginevyo hii nayo ni futuhi tuu kama futuhi zingine nyingi
ReplyDeleteAsilimia sabini za habari za hii blog ni mapishi so msomaji inabidi utumie uwezo wa ubongo wako kuchambua pumba na mchele
ReplyDeleteKweli
DeleteKama ni futuhi futuhika na wewe tukuone.
ReplyDeleteZipo timu nyingi likini yenye jina ni yanga pekeyake zingine hazina majina
ReplyDeleteUtopolo washindia mihogo, wanataka wapewe kwamkopo Kama makambo
ReplyDelete