December 13, 2020

 


KOCHA Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema kuwa kwenye mchezo wa leo dhidi ya Mbeya City anaweza kumpa nafasi mshambuliaji wake Chris Mugalu ambaye alikuwa anasumbuliwa na majeraha.


Leo Desemba 13, Simba inakibarua cha kusaka pointi tatu muhimu dhidi ya Mbeya City inayopambana kujinasua kutoka kwenye mstari wa kushuka Daraja.

Ikiwa imecheza mechi 14 imekusanya pointi 12 na inashika nafasi ya 15 inakutana na Simba iliyo nafasi ya tatu na pointi 26 baada ya kucheza mechi 12.

Sven amesema :-"Tumekuja na wachezaji 21 na wote wapo tayari kwa mchezo wetu. Mbeya City ni timu hatari, hawajapoteza kwenye michezo mitano iliyopita hivyo lazima tuwe vizuri zaidi ili tuweze kuibuka na ushindi.


"Nategemea kumtumia Mugalu kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City ninadhani anaweza kuanza benchi kisha nitampa nafasi ya kucheza ili ajenge hali ya kujiamini," amesema.


Kwenye Ligi Kuu Bara, Mugalu ametupia jumla ya mabao matatu kati ya 31 ambayo yamefungwa na Simba kwa msimu wa 2020/21.

4 COMMENTS:

  1. Kocha unambana sana huyo jamaa mugalu Leo ungemuamzisha japo DKK 60 ili tuone ana kitu ila unapomga DKK 15 unamkosea heshma bac tu ila mi najua jamaa najua kufunga sana tu by kelvin bara

    ReplyDelete
    Replies
    1. Atamuanzishaje mtu ametoka majeruhi ya muda mrefu!

      Delete
  2. Mugalu Ni mchezaji mzuri sema majeruhi yanamwandama

    ReplyDelete
  3. Mugalu Ni mchezaji mzuri sema majeruhi yanamwandama

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic