December 22, 2020


 NYOTA wa FC Lupopo Mpiana Moziz ametua ndani ya Bongo kwa ajili ya kumalizana na mabosi wa Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu George Lwandamina. 

Mshambuliaji huyo amekuja leo Desemba 22 akitokea nchini Congo na kesho Desemba 23 anatarajiwa kufanyiwa vipimo ambapo akifuzu atasaini dili la mwaka mmoja.

Amekuja kuchukua nafasi ya aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo Thiery Akono raia wa Cameroon ambaye ameuzwa na Klabu ya Azam FC na kuibukia nchini Malysia kwenye Klabu ya Negeri Sembilan.


Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa mpango mkubwa ni kuona kwamba kikosi kinarejea kwenye ubora wake kwa kupata wachezaji makini.


"Tumemleta Moziz ndani ya Bongo ambapo mpango wetu ni kumfanyia vipimo vyote pamoja na kucheki utimamu wake ikiwa kila kitu kitakuwa sawa atasaini mkataba wa mwaka mmoja ndani ya Azam FC,".

5 COMMENTS:

  1. Hongera Azam, huo mpira mnatoa mashine mnaingiza mashine

    ReplyDelete
  2. Hata walete mashine gan washapotea mazima

    ReplyDelete
  3. Bado wana nafasi ukizingatia kuwa hii ndo kwanza round ya kwanza inaishia

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic