December 1, 2020


 IMEELEZWA kuwa nyota wa Simba, Charlse Ilanfya yupo kwenye hesabu za kutolewa kwa mkopo ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Sven Vandenbroeck huku timu yake ya zamani ya KMC ikitajwa kuwa miongoni mwa zile ambazo zinamhitaji pamoja na Yanga.

Ilanfya ambaye kabla ya kuibukia ndani ya Simba kwenye usajili wa dirisha kubwa msimu huu alikuwa kwenye hesabu za kutua Yanga msimu wa 2018/19 kabla ya dili lake kubuma na kuibukia ndani ya KMC na sasa yupo zake Simba.

Habari zinaeleza kuwa kutokana  na kuwekwa benchi ndani ya Simba kwa kuwa nafasi anayocheza ina washambuliaji tengemeo ambao ni John Bocco na Meddie Kagere amekuwa akiishia benchi.

Kwenye mechi 11 ambazo Simba imecheza ameanza kikosi cha kwanza mechi moja ilikuwa mbele ya Tanzania Prisons jambo ambalo linamfungulia njia ya kuomba kutoka kwa mkopo.

 Ilanfya kuhusu jambo hilo amesema kuwa:”Bado sijapata taarifa rasmi na kuhusu kuomba kuondoka kwenda KMC ama Yanga hilo siwezi kulizingumzia kwa sasa,” .

Msimu uliopita akiwa ndani ya KMC alifunga mabao sita na kutoa pasi tatu za mabao jambo lililowafanya Simba kuisaka saini yake.

Kwa upande wa KMC, Christina Mwagala, Ofisa Habari wa timu hiyo amesema kwamba bado hawajapata taarifa kuhusu Ilanfya kutakiwa ndani ya kikosi hicho.

6 COMMENTS:

  1. Tutamrudisha KMC kwa mkopo,kwenda utopolo msahau.

    ReplyDelete
  2. Mwandishi nae ni kuma tu, hizo taarifa za kubuni fikia hatua uziache tu, YANGA haina mda wala uhitaji wa Ilanfya

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha matusi ww utopolo huna vhakuchangia kaa kimya

      Delete
    2. Bwana mdogo inaelekea ufahamu wako katika masuala ya mtandao ni mdogo sana.Unadhani ukiweka option ya "unknown" ndo utakosa kujulikana!!!Matusi peleka kwenye blog za wapuuzi wenzio na sio hapa.Waulize wajuzi wa mambo ya IT watakufahamisha

      Delete
  3. Jaman tuweke staha. Hata kama unajiona unknown unajulikana sana, hapa tutaniane, tubishane, tupeane changamoto lakin tusifikie huko; matusi?!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic