UONGOZI wa Klabu ya Yanga umethibitisha kuwa mshambuliaji wake mpya Saido Ntibazonkiza atawasili nchini kesho Jumatano usiku.
Nyota huyo ambaye alisajiliwa kwa dili la miaka miwili akiwa mchezaji huru ni tegemeo ndani ya kikosi cha timu ya Taifa ya Burundi akiwa ametupia jumla ya mabao matatu kwenye mechi za kufuzu Afcon.
Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa lengo la kumleta nyota huyo ni kuendeleza kasi ya timu hiyo kufikia malengo yao.
Huu unakuwa ni usajili wa kwanza kukamilika mapema kuelekea dirisha dogo ambalo linatarajiwa kufungulia Desemba 15.
Ataungana na kikosi cha Yanga kilichoweka kambi Kigamboni kikiwa chini ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze.
"Kila kitu kipo sawa, mshambuliaji wetu anakuja ndani ya Yanga, kesho Jumatano saa 3:20 usiku atakuwa ashatia timu uwanja wa ndege, hivyo kama ilivyo kawaida yetu mashabiki wa Yanga tujitokeze kwa wingi kumpokea," amesema.
Haya, nendeni airport mkampokee mwingine, maana wale waliopata mapokezi ya kihistoria wanachofanya uwanjani hakieleweki kabisa
ReplyDeleteKwani ww kinakuuma nini Yanga wanapofanya mambo yao hata kama hayaleti tija? Au ndio husda ndiyo inayokusumbua? Achana na mambo yasiyokuhusu
Delete@Waziri Usipate tabu Itakuwa husda tu
ReplyDeleteSawa sawa. Tumuache atapata aibu yeye mwenyewe
Delete@Waziri masamehe bure,
ReplyDeleteBaadhi ya binadamu ndivyo walivyo, hawapendi wengine wawe na raha
Kweli kabisa
DeleteWanachokifanya hakieleki? Timu inaongoza ligi mlitaka waihamishe Yanga iende wap?
ReplyDeleteMtambo wa mabao!!! Ngoja tusubiri mtambo uanze kukoboa nyavu. Raha jipe mwenyewe bwana.
ReplyDeleteMikia wanakereka sana kuona sisi tupo mbali nao. Kuwa na magoli mengi bila point za kutosha ni ufala tu😁😁😁😁😁😁😁😁
ReplyDelete