December 1, 2020


 BAADA ya kuwasili Tanzania leo Desemba Mosi kikitokea nchini Nigeria ambapo kilikuwa na mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Plateau United, kikosi cha Simba kinatarajia kutua Dar usiku.


Kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck leo kilitia timu Kilimanjaro majira ya 10 jioni na kiliweza kufanya mazoezi kwa ajili ya kuweka miili sawa ya wachezaji.


Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa New Jos nchini Nigeria Novemba 29, Simba ilishinda bao 1-0 hivyo ina kibarua cha kusaka ushindi Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa marudio.


Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Desemba 5, Uwanja wa Mkapa kisha ikiwa itashinda jumlajumla itapata nafasi ya kushiriki hatua ya mtoano.


Sven ameweka wazi kwamba furaha waliyopata baada ya ushindi nchini Nigeria inabidi iwe kwa kiasi kwa kuwa wana kazi nyingine Uwanja wa Mkapa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic