NYOTA wa Yanga, Carlos Fernandes ‘Carlinhos’ raia wa Angola yupo hatarini kukosa michezo yote mitatu iliyosalia ya raundi ya kwanza kutokana na majeraha ya nyonga aliyoyapata kwenye mchezo dhidi ya Namungo.
Carlinhos mwenye mabao mawili na pasi mbili za mabao hapo awali alikuwa akisumbuliwa na jeraha la kisigino lililomfanya akose michezo mitano alirejea na kufunga bao kwenye mchezo dhidi ya Namungo Novemba 22, mwaka huu.
Baada ya kupona majeraha hayo, Carlinhos amepata majeraha ya nyonga ambayo yamemfanya akose michezo mitatu mfululizo dhidi ya Azam, JKT Tanzania na mchezo uliopita dhidi ya Ruvu Shooting.
Daktari wa Yanga, Shecky Mngazija amesema: “Ni kweli mchezaji wetu, Carlos Fernandes ‘Carlinhos’ anaendelea na matibabu baada ya hivi karibuni kufanyiwa tena vipimo vya afya ambavyo vimeonyesha wazi bado afya yake haijatengemaa na ataendelea kuwa kwenye uangalizi wa madaktari.
“Mpaka sasa hatuna uhakika wa muda rasmi ambao atakuwa nje ya uwanja kwa sababu hii itategemea sana na kasi ya uponaji wa majeraha aliyonayo, lakini kuna uwezekano mkubwa akakosekana kwenye michezo mitatu iliyosalia ya mzunguko wa kwanza,” amesema Mngazija.
Chanzo: Championi








Dogo vipi mbona majeriho yanaelekea kumzoea? Aongeze lishe na umakini ili kujilinda
ReplyDeleteMajeruhi
ReplyDeleteMajeraha
DeleteKashapigwa misumari huyo. Chezea wananchi weyee!!
ReplyDeleteYanga hawana mchezaji kutoka Lindi....kule ambapo sasa hivi kunasifika kwa mitulinga.Nadhani umenielewa na kama hujanielewa kamuulize naibu waziri mteuliwa/mtenguliwa au mzee mzima mwenyewe
DeleteCha ajabu utakuta analipwa mshahara mkubwa kuliko Fei Toto au Kibwana Shomari au Yasin Mustafa wanaocheza kila mechi. Wabongo tuache dharau kwa wabongo wenzetu hao wanaokuja kukaa benchi watalipwaje zaidi ya wazawa? Mechi za mwanzo oooh hajazoea mazingira sasa oooh nyonga inamsumbua. Kwani Yanga wamemtoa timu gani au alikuwa mchezaji huru?
ReplyDeleteMchezaji ana kilo 40 atacheza wapi mpira!
ReplyDeleteNakubaliana na jamaa aliyesema tuthamini wachezaji wetu.Hapa Yanga tumeingizwa chaka. Tumeuziwa mzigo bila kuukagua.
Carlinhos sio dogo mnadanganywa na sura hiyo nyie .. mtu ashacheza misimu kibao huko kwao kameshachoka hako kababu
ReplyDelete