KOCHA wa Barcelona, Ronald Koeman, anaamini kuwa Barcelona itafanya kitu kuona msimu ujao Lionel Messi anacheza tena na Neymar ndani ya Camp Nou.
Hii ni baada ya hivi karibuni, Neymar kutamka wazi kuwa msimu ujao anataka kucheza tena na Messi ingawa haijaelezwa wapi kama ni PSG au Barcelona.
Neymar aliondoka Barcelona mwaka 2017 na kutua PSG. Alicheza na Messi ndani ya Barcelona kuanzia 2013, tangu msimu uliopita, staa huyo amekuwa akihusishwa kurejea viunga vya Camp Nou.
Nyota Messi mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu ambapo awali naye alikuwa anahitaji kusepa ndani ya kikosi hicho.
“Kila mmoja anafahamu suala la Messi, mtu pekee ambaye anayeweza kuamua hatma yake kwa sasa ni yeye mwenyewe.
“Klabu inapambana kuona inakuwa na wachezaji bora , nataka kuona Messi anacheza hapa na mchezaji bora (Neymar) ndani ya Camp Nou itakuwa vizuri zaidi,” amesema Koeman.
0 COMMENTS:
Post a Comment