December 7, 2020

 


KIKOSI cha Yanga kimeipoteza Simba kwa msimu wa 2020/21 kwa kuvuna pointi nyingi ugenini kwenye mechi sita ambazo wamecheza sawa na watani zao wa jadi ndani ya ligi.


Ikiwa ipo nafasi ya kwanza na pointi 34 baada ya kucheza mechi 14 na Simba ikiwa nafasi ya tatu ikiwa na pointi 23 kabla ya mechi za jana, chini ya Sven Vandenbroeck mambo yamekuwa magumu kupata pointi tatu ikiwa ugenini.


Simba imecheza jumla ya mechi sita ambazo ni dakika 540 ugenini huku ikishinda mechi tatu, sare mbili imeambulia kipigo mechi moja mbele ya Tanzania Prisons. Ilikuwa ikisaka pointi 18 imeambulia pointi 11 na kupoteza pointi saba ugenini.


Mwendo wake ulikuwa namna hii:-Septemba 6, Ihefu 1-2 Simba, Uwanja wa Sokoine, Septemba 12, Mtibwa Sugar 1-1 Simba,Uwanja wa Jamhuri, Moro Oktoba 4, JKT Tanzania 0-4 Simba, Uwanja wa Jamhuri,Dodoma, Oktoba 22, Tanzania Prisons 1-0 Simba, Uwanja wa Nelson Mandela, Novemba 7, Yanga 1-1 Simba, Uwanja wa Mkapa na Coastal Union 0-7 Simba, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.


Yanga ambayo inanolewa na Cedric Kaze imecheza mechi sita pia ugenini ambazo ni dakika 540. Imeshinda mechi tano na kulazimisha sare ya bila kufungana na Gwambina FC, ikiwa inasaka pointi 18 imesepa na pointi 16 na kuyeyusha pointi mbili ugenini.


Mwendo wake ulikuwa namna hii:-Septemba 19, Kagera Sugar 0-1 Yanga, Uwanja wa Kaitaba, Septemba 27,Mtibwa Sugar 0-1 Yanga, Uwanja wa Jamhuri, Moro, Septemba 25, KMC 1-2 Yanga, Uwanja wa CCM Kirumba, Septemba 31, Biashara United 0-1 Yanga, Uwanja wa Karume.


Novemba 3, Gwambina 0-0 Yanga, Uwanja wa Gwambina Complex na Novemba 25, Azam FC 0-1 Yanga, Uwanja wa Azam Complex.

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic