December 2, 2020

 


Cecafa U 20

FT


 TIMU ya Taifa ya Tanzania chni ya miaka 20, Ngorongoro Heroes leo Desemba 2 imepoteza ubingwa wa mashindano ya Cecafa dhidi ya Uganda kwa kufungwa mabao 4-1.


Mchezo wa leo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa Uwanja wa Black Rhino ulishuhudiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF), Wallace Karia ambaye ni Rais pia wa Cecafa.

Mabao ya Uganda yalifungwa na Richard Basangwa dakika ya 12, Steven Sserwadda dk 44 ,Ivan Bogere 61  na Kenneth Semakula 72.

Bao la Tanzania lilifungwa na Abdul.H.Suleiman dk 30 kwa mkwaju wa penalti na kuwafanya Uganda wasepe na taji hilo ambalo lilikuwa mikononi mwa Ngorongoro Heroes.


8 COMMENTS:

  1. Replies
    1. Hapa watanzania ndipo tunapokosea kwa vijana wetu.Hapa ndipo serikali na TFF walipaswa kuwa makini kwa kutafuta kocha bora wa kukuza vipaji sio ilimradi kocha.

      Delete
  2. 4-1 Kuna ushindani gani?nilisema huku walikutana Na timu dhaifu Djibut,Somalia,sudani kusini,nchi za njaa nq vita

    ReplyDelete
  3. siyo mbaya jipangeni na mashindano yajayo. Uwezo mnao ndiyo tegemeo letu la Baadae👋

    ReplyDelete
  4. Zuberi Katwila alileta kombe na timu hii nje ya nchi Jamhuri Kiwelo kaja kulipoteza hapa hapa nchini.

    ReplyDelete
  5. Kwahyo unataka libaki? Kalikatalie uwanja wa ndege

    ReplyDelete
  6. Kwa kweli inahuzunisha sana. Vijana wa Ngorongoro Heroes ni wazuri na wana vipaji vya hali ya juu vya soka. Hapana shaka kwamba matarajio ya watanzania wengi yalikuwa kwamba Heroes wangechukua Ubingwa huu kwa mara ya pili mfululizo. Kufungwa kwao kwa kiasi kikubwa naamini kunatokana na aina ya kocha waliye naye. Naamini huyu sio kocha sahihi kwa timu za vijana. TFF wajifunze katika hili lililotokea na wawaandalie vijana makocha mahiri wa timu za vijana. Tayari tuna rekodi nzuri kwa makocha kama Zuberi Katwila na Bakari Shime "Mchawi Mweusi". Hawa wawili kwa pamoja wapewe hii timu waiandae vizuri kwa ajili ya AFCON 2021. Naamini vijana watafanya maajabu kwa makocha hawa. Nawasilisha.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic