HOMA imezidi kupanda kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaozikutanisha Klabu za Yanga na Ruvu Shooting siku ya Jumapili.
Tayari wenyeji wa mchezo huo Yanga wamesisitiza kuwa wanataka pointi tatu muhimu kwenye mchezo huo, hivyo hawatawadharau wapinzani wao.
Akizungumza na Saleh Jembe, Meneja wa kikosi cha Yanga, Hafidh Saleh amesema wanajua Ruvu Shooting ni miongoni mwa timu ngumu ndani ya Ligi Kuu Bara kutokana na ubora wa kikosi walichonacho.
"Mbele yetu tuna mchezo mgumu dhidi ya Ruvu Shooting ambao tunatarajia kucheza nao siku ya Jumapili, tunajua utakuwa mchezo mgumu kutokana na umuhimu wa kupata matokeo chanya kwenye mchezo huu hivyo hatuwezi kuidharau Ruvu.
"Tayari kikosi kipo kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huu ambapo tulianza rasmi kambi siku ya Jumanne na taarifa njema kwetu ni kurejea kwa baadhi ya nyota wa kikosi chetu waliokosa mchezo uliopita dhidi ya JKT Tanzania akiwemo, Kibwana Shomari," .
Yanga imecheza jumla ya mechi 13 ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 31, inakutana na Ruvu Shooting, Desemba 6 Uwanja wa Mkapa.
Ruvu Shooting ipo nafasi ya nne kibindoni ina pointi 23.
Msituzuge wakati tunajua kuna agent wenu mkwasa na bwire washaweka mambo sawa
ReplyDeleteMikia fc hamna namna yoyote mavi yanagonga chupi, nguruwe fc bwana
ReplyDeleteUnasemaje nyani fc wazee wa kuoonewa
DeleteAkili zako ndogo,bingwa Nani mpaka sasa kombe analo Nani. Ninyi endeleeeni kucheza Cha ndimu Wanaume wakisakata kabumbu la kimataifa
Delete