December 16, 2020


 UONGOZI wa KMC umesema kuwa utacheza pira spana mbele ya Simba na kusepa na pointi tatu muhimu ndani ya Uwanja.


Simba itawakaribisa KMC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Mkapa huku kila timu ikitamba kusepa na pointi tatu muhimu.


Mchezo wao wa mwisho msimu uliopita kukutana uwanjani, Simba ilishinda mabao 2-0 hivyo leo KMC itaingia uwanjani ikiwa na hesabu za kulipa kisasi.


Pia KMC bado ina maumivu ya kuyeyusha pointi tatu dhidi ya Mtibwa Sugar baada ya kufungwa bao 1-0 huku ikitambua kwamba inakutana na Simba ambayo imetoka kushinda bao 1-0 dhidi ya Mbeya City.

Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema""Ipo wazi na tunatambua kwamba tunakutana na Simba ikiwa imetoka kushinda mbele ya Mbeya City huko Mbeya.


"Walishinda mbele ya Mbeya City sasa wanakutana na Kino Boys, tutacheza pira spana, pira kodi, pira mapato lengo ikiwa ni kupata pointi tatu.


"Mashabiki wajitokeze kwa wingu kutupa sapoti ili kuona namna gani tunaondoka na pointi tatu muhimu," .


KMC ipo nafasi ya tano ikiwa na pointi 21 inakutana na Simba iliyo nafasi ya pili na pointi 29.

7 COMMENTS:

  1. Utashangaa leo KMc wanapanga Team hovyo kiss kuwapa Simba nafasi,Kama hamwamini subiri,ndiyo maana hata Salehe hajatoa lineup watakula Kama za Coastal mamluki Hawa .

    ReplyDelete
  2. Jamani wabongo kwa kuiga mmebarikiwa tokea Simba aanze pira biriani sasa wengine ndo hao wanakuja na pira spana mara pira mapato duh!!!

    ReplyDelete
  3. Kweli nilitabiri hii Timu imelaaniwa na Usimba,ndiyo maana wakatupeleka mwanza ukiangalia line up wamepanga Timu dhaifu na ukiangalia hawataki kupiga mpira against Simba mfumo .Simba wanahitaji kukimbizwa hawawezi soukous

    ReplyDelete
  4. Hata Mtangazaji Kama kapangwa anajua muda was goli bt Wananchi tumewekeza vitangazi vya Azam moja ya Itikadi yao sifia/Saidia /Elekeza ili mradi Simba apate advantage

    ReplyDelete
  5. Angalia hata sub,kweli Ile ya Siasa ipo mpirani

    ReplyDelete
  6. Sikia matako Kaseja sasa tusubiri Wachambuzi na Makocha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic