WAKATI leo Azam FC ikitaiwa kushuka uwanjani kumenyana na Gwambina FC nyota wake watatu wanatarajia kuukosa mchezo wa leo kutokana na kusumbuliwa na majeraha.
Ikiwa chini ya kocha msaidizi, Vivier Bahati baada ya kumfuta kazi, Arstica Cioaba Novemba 26 siku moja baada ya kufungwa na Yanga bao 1-0 Uwanja wa Mkapa itashuka tena uwanjani saa 10:00 Uwanja wa Gwambina Complex.
Nyota hao ni pamoja na Nivere Tigere, Yakub Mohamed, Sure Boy na mtupiaji wao namba moja Prince Dube ambaye yupo Afrika Kusini akipewa huduma baada ya kuumia mkono.
Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa wanaamini watapambana kusaka pointi tatu kwenye mchezo wa leo.
0 COMMENTS:
Post a Comment