December 7, 2020


 UONGOZI wa KMC umesema kuwa kwa sasa akili zote ni kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar unaotarajiwa kuchezwa Desemba 11.


Mchezo huo utachezwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro yalipo makao makuu ya timu hiyo kongwe ndani ya ardhi ya Bongo.


Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa tayari kikosi kimeanza maandalizi ili kuweza kupata ushindi kwenye mchezo wao.


"Kwa sasa kikosi kimeanza maandalizi kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Mtibwa Sugar na tuna amini kwamba tutapata matokeo chanya ndani ya uwanja.


"Tunaamini kwamba mchezo utakuwa mgumu ila tupo tayari hasa ukizingatia kwamba kwa sasa wachezaji wamekuwa na shauku ya kupata ushindi ndani ya uwanja.


"Mashabiki waendelee kutupa sapoti imani yetu ni kwamba tutafanya vizuri na kila kitu kinawezekana," amesema.


Timu zote zinakutana uwanjani zikiwa zimetoka kushinda mechi zao zilizopita ambapo KMC ilishinda bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji na Mtibwa Sugar ilishinda bao 1-0 dhidi ya Mwadui FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic