December 1, 2020


 NYOTA wanne wa Klabu ya Yanga wanapambania tuzo ya mchezaji bora kwa mwezi Novemba ambao umekamilika jana.


Ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 31 baada ya kucheza mechi 13.


Wachezaji hao wanaowania tuzo hiyo ni pamoja na kipa namba moja Metacha Mnata ambaye amecheza jumla ya mechi 12 kati ya 13 na beki chipukizi, Bakari Mwamnyeto.

Pia yupo kiraka Deus Kaseke ambaye amefunga jumla ya mabao mawili kwenye mechi mbili mfululizo ilikuwa mbele ya Azam FC na JKT Tanzania.


Mshambuliaji mwenye spidi ila hana bahati ya kufunga naye yumo kwenye orodha hiyo ambaye ni Yacouba Songne mwenye bao moja na pasi mbili za mabao.


Ili kumpigia kura mchezaji unayempenda, Yanga wameweka utaratibu kwamba unampigia kura kupitia akaunti yao ya Twitter,'yangasc1935'.

4 COMMENTS:

  1. Sasa huyo mwenye speed na hajafunga bao hata moja ndio anagombea tunzo kwasababu Ana speed.

    ReplyDelete
  2. Hamna kitu hapo utopolo mtupu hadi mwandishi mtopolo tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic