December 5, 2020


 IKIWA leo Uwanja wa Mkapa, timu ya Plateau United inamenyana na Simba kwenye mchezo wa marudio wa Ligi ya Mabingwa Afrika timu hiyo imemtaja mchezaji ambaye aliwapa tabu Novemba 29, Uwanja wa New Jos.


Kwenye mchezo wa kwanza Simba ilishinda bao 1-0 ambalo lilipachikwa na Clatous Chama, jambo ambalo limewafanya waje Bongo kwa tahadhari.


Nahodha wa Klabu ya Plateau United ya Nigeria, Golbe Elisha amesema kuwa ni mchezaji mmoja hivi mweusi halafu mfupi anacheza kwa juhudi uwanjani aliwavuruga namna alivyotaka ndani ya uwanja.

"Yule aliyetoa pasi ya bao mweusi ana nguvu halafu mfupi hata nafasi yake sijui ilikuwa ni ipi maana alikuwa anafanya namna anavyotaka akiwa uwanjani, ni mchezaji ambaye alikuwa anafanya anavyojua ni yule aliyetoa pasi ya bao nilimuona,(Luis Miquissone).

"Tumekuja Bongo tunajua kwamba mchezo utakuwa mgumu lakini tumejipanga kuona namna gani tutapata matokeo kwenye mchezo wetu," amesema.

5 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic