KIUNGO wa Manchester United, Paul Pogba ametuma ujumbe ambao umeonekana kuwa ni kijembe kwa Legendi wa Manchester United, Gary Neville na Roy Keane ambao kwa pamoja walimtumia ujumbe kiungo huyo Jumamosi iliyopita kwamba anatakiwa kuachwa.
Nyota hao wa zamani wa Manchester United walisema kuwa ni muda sahihi wa United kumuacha Pogba aondoke ndani ya kikosi hicho kwa sababu wakala wake Mino Raiola alisema kuwa hana furaha ndani ya kikosi hicho.
Muda mfupi baada ya maoni hayo kwenye sare ya bila kufungana kwa Manchester United na Manchester City uliochezwa Uwanja wa Old Trafford, Pogba ambaye alianza pia kikosi cha kwanza alituma ujumbe kupitia ukurasa wake wa Istagram kwa kuwataka watu wasiojua mambo ya ndani kukaa kimya kwa kuwa hana tatizo na Manchester United.
"Muda wote napambana kwa ajili ya Manchester United, mashabiki na wachezaji wenzangu wote tunapeana sapoti. Bla bla sio kitu cha muhimu. Malengo yangu yapo mbali kila siku.
"Asilimia 1,000 ninahusika katika mipango kazi ya Manchester United, muda wote nimekuwa muwazi na kila kitu kinakwenda sawa. Ikiwa haujui kinachoendelea ndani usiongee," .
0 COMMENTS:
Post a Comment