December 21, 2020

 


RUVU Shooting kwa msimu wa 2020/21 imeweka rekodi ya kuwa timu pekee iliyo ndani ya tano bora ikiwa chini ya Kocha Mkuu,  Charles Mkwasa ambaye ni mzawa.

Nafasi ya kwanza ipo  kwa Mrundi Cedric Kaze wa Yanga akiwa na jumla ya pointi 40 baada ya kucheza mechi 16.

Nafasi ya pili ipo kwa Mbeligiji Sven Vandenbroeck wa Simba akiwa na pointi 32 baada ya kucheza mechi 14, nafasi ya tatu ipo kwa George Lwandamina wa Zambia ndani ya Azam FC ikiwa na pointi 29 baada ya kucheza mechi 16.

Nafasi tano ipo kwa Biashara United inayonolewa na Francis Baraza wa Kenya akiwa na pointi 23 baada ya kucheza mechi 16.

Mbali na kuwa na kocha mzawa pia wachezaji wake asilimia 100 ni wazawa na wanaonyesha uwezo mkubwa wa kusaka pointi tatu ndani ya uwanja bila kukata tamaa.


Nahodha wa kikosi hicho ni Fully Zully Maganga ambaye amesema kuwa wachezaji wamejipa kazi ya kusaka ushindi kwenye kila mchezo watakaoingia ndani ya uwanja.

Mkwasa ni mzawa wa kwanza kwa msimu huu kutwaa tuzo ya kocha bora wa mwezi, alitwaa ile ya Novemba ambapo Septemba ilikuwa mikononi mwa Aristica Cioaba raia wa Romania na Oktoba ilisepa na Cedric Kaze wa Burundi.  



2 COMMENTS:

  1. record lazima iwe kitu special sio kila kitu ambacho mtu amefanikiwa kukipata na kwa kuwa wengine hawajakipata basi.Sio kwamba zikipita siku saba katika wiki mvua haijanyesha badi unasema wiki hiyo imeweka rekodi..mambo mengine unayoandika ni upuuzi..
    afadhali hata wangekuwa nafasi ya tatu kidogo ingeleta mmaana..hivi kweli umeenda chuo ukajifunza critical thinking? ujue unavyoandika hapa wasomaji wengi wanakupima uwezo wako wa kufikiri na kuelewa.Rudi shule

    ReplyDelete
  2. Mkwasa alishawahi kuwa kocha wa Timu ya Taifa! Je unadhani angekuwa na kikosi kama cha Yanga au Simba au Azam bado angekuwa kwenye rekodi hiyo...fikiria utaelewa sio kushangaa kila jambo kama ni rekodi.,Inaonekana mtu akiwa ndiye pekee kavaa shati la bluu kazini kwako...basi ameweka rekodi..akili yako ndiyo imeishia hapo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic