December 21, 2020


 IMEELEZWA kuwa Yanga ipo kwenye mchakato wa kumshusha Jacques Tuyisenge na kumtoa kwa mkopo staa wao kipenzi, Carlos Carlinhos.

 

Awali, Yanga ilidaiwa kumtaka Tuyisenge anayekipiga APR ya Rwanda kwenye dirisha kubwa wakati huo alikuwa ametoka kusitisha mkataba wake na Petro Luanda ya Angola lakini dili lilishindikana na wababe wa Jangwani wakamshusha Michael Sarpong.

 

Habari zinaeleza kuwa mabosi wa Yanga wameamua kurejea tena kujaribu kumsajili Tuyisenge ambaye ni rafiki wa mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere na walicheza pamoja Gor Mahia ya Kenya.


Chanzo hicho kiliongeza kuwa, tayari viongozi wameanza mchakato wa kuwasiliana na APR ili waweze kupewa Tuyisenge ambaye kwa mujibu wa mtandao wa Transfermarket, mkataba wake unaisha Juni 30, 2022.

 

Inadaiwa kuwa, kama wakifanikisha dili hilo haraka kwenye usajili huu wa dirisha dogo uliofunguliwa Desemba 16, atakuja kuchukua nafasi ya Carlinhos ambaye watamtoa kwa mkopo.

 

“Tayari tumewasiliana nao viongozi wa APR na kama watakubaliana na ofa yetu kwa Tuyisenge basi kuna uwezekano mkubwa wa kuachana na Carlinhos ambaye tutamtoa kwa mkopo ili tuweze kupata straika mwenye uwezo wa kupambana kama ilivyo kwake (Tuyisenge).

 

"Msimu huu tunatakiwa kupata ubingwa hivyo tunaweka nguvu kubwa katika kuhakikisha tunapata mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa wa kufunga kama Tuyisenge, hivyo muda si mrefu tutajua matokeo ya ofa yetu hiyo kutoka APR,” kilisema chanzo hicho.


Chanzo:Championi

4 COMMENTS:

  1. Acha kuvuruga timu kwa habari za uongo, mshambuliaji anachukuaje nafasi ya kiungo!! Yanga in nafasi moja ya mchezaji wa nje na ukiongeza ya Morrison zinakuwa mbili

    ReplyDelete
  2. Mbona mmesahau Chama naye si ni mchezaji wenu

    ReplyDelete
  3. Hakika viongozi walithibitisha hilo hadi tukawekewa video Chama akiwa kwenye jezi ya Yanga huku akitangaza jarida la klabu hiyo. Dismas Ten anajua vizuri. "Time will tell" alituaminisha Nugaz

    ReplyDelete
  4. Safi sana huo ndio utani wa jadi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic