UONGOZI wa Ruvu Shooting umesema kuwa mchezo wao dhidi ya Yanga, Desemba 6 Uwanja wa Mkapa watapambana kupata pointi tatu kwa kuwa wamedhamiria kufanya hivyo.
Yanga ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 31 baada ya kucheza mechi 13 inakutana na Ruvu Shooting yenye pointi 23 baada ya kucheza mechi 13 ikiwa nafasi ya nne kwenye msimamo.
Kwa msimu wa 2019/20 timu zote ngoma ilikuwa ni ngumu kwa kuwa hakukupatikana mbabe ndani ya dakika 180 walizokutana uwanjani kwa kila timu kusepa na pointi tatu mchezo mmoja.
Mchezo wa mzunguko wa kwanza Ruvu Shooting ilisepa na pointi tatu na ule wa pili Yanga ilisepa na pointi tatu hivyo Desemba 6 wanaanza upya kusaka mbabe mpya.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting Masau Bwire amesema kuwa hawatanii ila watafanya kweli kwenye mchezo wao dhidi ya Yanga.
"Unajua wengi wanafikiri labda tunatania hapana, sina utani katika hili nina amini kwamba tunakwenda uwanjani kusaka ushindi na tutashinda kweli.
"Tutaingia uwanjani tukiwa na hesabu za kupata pointi tatu, mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti," amesema.
Muangusheni chali Gongo
ReplyDeleteKisa ulipigwa wewe unadhani na yanga atafungwa mikia bwana ovyo
DeleteYanga hii? Asiifananishe na maveteran fc au mbeya city masau atapigwa tuu
ReplyDelete