December 4, 2020

 


KLABU ya KMC leo Desemba 4 imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Uhuru.

Ikiwa na sera ya pira spana, pira mapato ilitumia dakika 45 za mwanzo bila kugusa lango la mpinzani na kuzifanya timu zote kwenda mapumziko zikiwa zimetoshana nguvu.

Kipindi cha pili KMC iliongeza kasi ya mashambulizi ambayo ilileta matunda kwao kwa kuweza kutumia nafasi moja waliyoipata.

Bao pekee la ushindi kwa KMC lilifungwa  na Emmanuel Mvuyekure dakika ya 58 baada wana Kino Boys kuliandama lango la Dodoma Jiji.


Mvuyekure alipachika bao hilo kwa kichwa akimalizia kona iliyopigwa kwa guu la kushoto na Ally Ramadhani.


Mvuyekure amesema kuwa maandalizi mazuri yamewapa matokeo na kusepa na pointi tatu muhimu.

1 COMMENTS:

  1. Kazeni buti ndug zangu me nataman sana mje kuchukua nafasi ya yanga maana hao jamaa mpira ushawashinda asaiv wanageukia masumbwi na ukahaba yan wao kila mgeni wanamshobokea vijana wanasema "JANVI LA WAGENI"

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic