December 30, 2020


 IMEELEZWA kuwa sababu ya nyota wa kikosi cha Simba, Jonas Mkude kusimamishwa na mabosi wa timu hiyo ni mfululizo wa makosa ya mara kwa mara ikiwa ni pamoja na unywaji pombe kupitiliza.

Kiungo huyo mkabaji Desemba 28 amesimamishwa na Simba huku akitarajiwa kupelekwa kamati ya nidhamu kujibu shutuma zinazomkabili.

Ndani ya Ligi Kuu Bara chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck kikosi hicho kikiwa kimecheza jumla ya mechi 14 yeye amecheza mechi 10 akikosekana kwenye mechi nne.

Katika mechi hizo 10 alizocheza moja alianzia benchi huku tisa akianza kikosi cha kwanza ndani ya timu hiyo inayopambana kutetea taji la ligi

Habari zinaeleza kuwa nyota huyo alikunywa kupita kiasi kabla ya timu yake kuvaana na FC Platinum ya Zimbabwe wakati Simba ikipoteza kwa kufungwa bao 1-0.

"Mkude amekuwa na tabia za kunywa kupita kiasi hata kabla ya mechi ngumu na muhimu, licha ya kuonywa amekuwa akirudia kufanya makosa hayo hata nchini Nigeria alifanya hivyo hata Zimbabwe.

"Pia amekuwa ni mwenye kununa kila mara kwa wachezaji wenzake na hata viongozi hivyo kwa sasa madai yake yanafanyiwa uchunguzi na yeye ataitwa kujibu," ilieleza taarifa hiyo.


Simba leo itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Ihefu na Januari 6 ina kazi ya kusaka ushindi mbele ya FC Platinum ya Zimbabwe.


6 COMMENTS:

  1. Kunywa anywee Zimbabwe uchunguzi Tanzania...

    ReplyDelete
  2. Hivi na kule Zimbabwe kuna pombe aina ya KOMONI kama huku? Hahahahahaha

    ReplyDelete
  3. Si mseme ukweli tu kwamba kaomba nonihino kwa boss; mbona vitu vya kawaida tu?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na yule mwingine "sura kavu" mbona ye hajachukuliwa hatua au kwa vile mpachikaji?

      Delete
  4. Mkude mlevi na kwa kiasi fulani unaweza kusema Simba ndio inayoyalinda maisha ya mkude.simba ni Kama mzazi mwema kwa mkude la sivyo mkude angekuwa pabaya zaidi alivyo sasa na kwa kiukweli sio Simba inayomuhitaji mkude bali mkude ndie anaeihitaji Simba tena sana,hakuna kiungo bora Ramadhani chombo Redondo pale Simba lakini alizimika ghafla nadhani kwa matatizo Kama mkude.

    ReplyDelete
    Replies
    1. umeongea neno; unakumbuka kisa cha nyoni kuanzia benchi msimu huu? NGONO KUPITILIZA ALIONYWA MARA KIBAO BUT HAKUSIKIA LKILICHOFUATA NI MKEKA MPAKA ALIPOJIRUDI MWENYEWE

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic