December 30, 2020


 UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting ambao utakuwa ni wa zmunguko wa pili.

Mchezo wa kwanza kwa msimu wa 2020/21 timu hizi zilitoshana nguvu ya bila kufungana na waligawana pointi mojamoja.

Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar,Thobias Kifaru amesema wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao utakuwa na ushindani mkubwa.

"Tuna mchezo mgumu na wenye ushindani mkubwa ila sisi tupo tayari na tunahitaji kupata pointi tatu muhimu ndani ya uwanja.

"Mchezo wetu wa kwanza tulitoshana nao nguvu na inatufanya tuzidi kujipanga kwa ajili ya mchezo wetu ujao, mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti," amesema.

Utakuwa ni mchezo wa kwanza ndani ya 2021 kwa timu hizi mbili kukutana ndani ya uwanja. Utachezwa Januari 2,2021.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic