December 1, 2020


BAADA ya kuanza vyema kampeni yake katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Plateau United ya Nigeria, kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Klabu ya Simba leo jioni kinatarajiwa kurejea nchini.

 

Bao la Simba katika mchezo huo wa awali ugenini lilifungwa dakika ya 53 ya mchezo na kiungo wa kimataifa wa Zambia, Clatous Chama akitumia vizuri pasi ya, Luis Miquissone ‘Konde Boy’.

 

Meneja wa kikosi cha Simba, Abbas Ally amesema kikosi kilianza safari jana alfajiri kutokea Jos, Nigeria kupitia Ethiopia na kinatarajia kutua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro majira ya saa 10:00 jioni.



 

“Tunashukuru kwa kuanza vizuri michuano hii mikubwa kwa ngazi ya klabu barani Afrika, licha ya matokeo ya ushindi tuliyoyapata nikiri kuwa haukuwa mchezo rahisi kutokana na ubora wa wapinzani wetu na hata mazingira ya mchezo, lakini wachezaji wetu walipambana sana kuhakikisha tunapata matokeo.

 

“Kikosi tayari kimeanza safari asubuhi kutoka Jos kuelekea Abuja, ambapo tutasafiri kwa ndege hadi Ethiopia ambapo tutapumzika na kuanza safari ya kurejea Tanzania siku ya Jumanne na tunatarajia kufika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro majira ya saa kumi jioni,” amesema Abbas.

 

Simba na Plateau zitarudiana Desemba 5 siku ya Jumamosi Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es salaam tayari kikosi kimeanza safari kutoka Abuja kurejea Tanzania.

 

Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa wana kazi ya kujiandaa kwa ajili ya mchezo wa marudio ambao anaamini kwamba utakuwa na ushindani mkubwa. 

 

 

 


3 COMMENTS:

  1. Cha muhimu tusilipe kiasi kutokana kwa walotufanyia. Tuwalipe wema na hiyo itakuwa ni adhabu kuliko kuwafanyia uovu. Kama waungwana itawaumiza kwasababu wanategemea watafanyiwa uovu. Sisi ni wastaarabu wenye kuheshimiwa. Mshinde adui wako kwa kufanya rafiki yako na Mungu yupo na ushindi ni wetu Inshallah. Hakuna kuzomea isipokuwa kumuomba Mungu

    ReplyDelete
  2. Mungu atawalipia CIE tube mungu tupate ushindi Fuji tuwaachie uto Fc simba in ushindi na pira biriani tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic