December 21, 2020


 UONGOZI wa Simba umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum ambao unatarajiwa kuchezwa Desemba 23, Uwanja taifa wa Zimbabwe.


Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili kutokana na umuhimu wake huku Simba ikiweka wazi kwamba imejipanga kupata matokeo chanya. 


Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa maandalizi ambayo wameyafanya yanawapa matumaini ya kuweza kupata matokeo ambayo wanayafikiria.

"Kikosi kipo imara na maandalizi yanakwenda vizuri huku na tunaamini kwamba kwa namna ambavyo tumejipanga tuna nafasi ya kupata matokeo.

"Kikubwa mashabiki wazidi kutuombea na kutupa sapoti ili tuweze kushinda mchezo wetu, benchi la ufundi linatambua kwamba mchezo utakuwa mgumu na wenye ushindani ila tupo tayari," .

Mchezo huo utachezwa majira ya saa 9:00 kwa saa za Zimbabwe ambapo kwa Bongo itakuwa saa 10:00 jioni. 

6 COMMENTS:

  1. Tunawatakia kila la kheri katika mchezo huo muhimu.

    ReplyDelete
  2. Kila la kheri ninyi ni wwawakilishi wa nchi mmebeba bendera ya taifa piganeni kama taifa

    ReplyDelete
  3. Simba wanaweza kushinda mechi hiyo ila wakizembea watakula nyingi. Wakaze msuli na kuheshimu wapinzani wao.

    ReplyDelete
  4. Mechi itakuangum mno japotunahtaji ushindi nilazima tucheze kwatahazal sana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic