December 21, 2020


 


UONGOZI wa Klabu ya Azam umeweka wazi kwamba kuna timu nyingi ndani na nje ya nchi ambazo zimetuma maombi yao kwa ajili ya kuwataka wachezaji waliopo ndani ya kikosi hicho ili waweze kupata huduma zao.

Azam FC licha ya kuwa kwenye mwendo wa kusuasua kwa msimu wa 2020/21 baada ya kuanza kwa kasi kwenye mechi 7 za mwanzo ambapo walishinda zote na kukusanya pointi 21 kwa sasa wanapambana kurejea kwenye ubora.

Mwendo mbovu kwenye mechi zao tano za hivi karibuni ulifanya uongozi umfute kazi, Kocha Mkuu Arstica Cioaba na kwa sasa mikoba ipo chini ya George Lwandamini.

Jana, Desemba 20 Azam FC ilikamilisha dili la nyota wake wa Cameroon, Alain Thierry Akono Akono kuelekea nchini Malaysia, ambapo nyota huyo anakuwa mchezaji wa tatu kuuzwa na Azam msimu huu baada ya Mshambuliaji,  Shaaban Idd Chilunda na kiungo mkabaji Novatus Dismas waliouzwa mwezi Oktoba.

Akizungumzia biashara hiyo ya wachezaji, Mkuu wa Kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Azam, Zakaria Thabith 'Zaka Zakazi' amesema:- "Baada ya kukamilisha usajili wa Alain Akono kumekuwa na maswali mengi kuhusu ofa za wachezaji wa klabu yetu kwa kuzingatia huyu ni mchezaji wa tatu tumemuuza msimu huu baada ya Shaaban Chilunda na Novatus Dismas.

"Ni kweli tuna ofa nyingi kutoka ndani na nje ya nchi ambapo kuna baadhi ya klabu zinawahitaji kwa mkopo, na wengine moja kwa moja hivyo nasi tunafanya tathimini na kama kuna klabu itakidhi vigezo basi tutawatangaza hivi karbuni,"

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic