December 13, 2020


MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara Klabu ya Simba, leo imetangaza mchakato mzima wa uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi ya mwenyekiti utakaoanza leo Desemba 13, na kutarajiwa kukamilika Februari 7, mwakani,

Nafasi hiyo kwa sasa anaikaimu, Mwina Seif Kaduguda baada ya kuachwa wazi na aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Swedi Mkwabi aliyejiuzulu wadhifa huo Septemba 14, mwaka jana baada ya kuhudumu kwa takribani miezi kumi pekee.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ndani ya klabu hiyo, Boniface Lihamwike amesema: "Tunataka kuwahakikishia Wanasimba na wadau wote wa michezo kiujumla kuwa uchaguzi huu utakuwa huru na wa haki.

Akitoa ratiba ya mchakato huo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati, Steven Ally amesema: "Mchakato wa uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi ya Mwenyekiti wa Klabu ya Simba umeanza rasmi leo baada ya taarifa hii, na utaendelea mpaka Februari 7, 2021 ambapo ndiyo tunatarajia kufanya uchaguzi na kutangaza mshindi wa nafasi hiyo.

"Kwa taarifa zaidi kuhusu mchakato mzima tumebandika ratiba hii makao makuu ya klabu lakini pia watu wanaweza kuipata kupitia mitandao yetu ya kijamii, vigezo vya kuchukua fomu ni vile ambavyo vimewekwa bayana na Ibara ya 27 ya katiba ya klabu na pia vinapatikana kwenye fomu.

"Lakini kwa uchache ni lazima mgombea awe na elimu ya angalau Shahada inayotambuliwa na tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU), na kadi ya mwanachama hai kwa miaka mitatu huku gharama kwa fomu ikiwa ni Shilingi laki tatu," .

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic