December 16, 2020


MAKAMU Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga na Mkurugenzi Uwekezaji wa Kampuni ya GSM, Injinia Hersi Said amesema kuwa wapo wachezaji ambao watatolewa kwa mkopo ili kulinda vipaji vyao.

Yanga ikiwa chini ya Kocha Mkuu Cedric Kaze imeendelea kuwa imara kwa kupata matokeo mazuri jambo ambalo limewafanya waendelee kuwa vinara na pointi zao 37.

Injia amesema kuwa wamepokea ripoti kutoka kwa kocha ambayo imetoa maelekezo ya kuwatoa nyota wengine kwa mkopo ili kupata nafasi ya kucheza na kuongeza uwezo.

Miongoni mwa nyota ambao watasepa ndani ya kikosi hicho ni pamoja na Juma Mahadhi huyu tayari ameshapelekwa Ihefu FC, Abdulaziz Makame,Adam Kiondo na Fahad Omar.

Pia inaelezwa kuwa mwingine ambaye huenda akatolewa kwa mkopo ni pamoja na beki Paul Godfrey, mshambuliaji Waziri Junior ambao wamekuwa hawana nafasi kikosi cha kwanza chini ya Cedric Kaze na kufanya idadi ya watakaopigwa panga kuwa sita.


Tayari dirisha dogo limefunguliwa jana Desembe 15 ambapo Yanga imekamilisha usajili wa nyota mmoja ambaye ni Saido Ntibanzokiza, raia wa Burundi akiwa ni mchezaji huru.


Nyota huyo amesaini dili la miaka miwili na jana kwa mara ya kwanza alicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Singida United na kutupia mabao mawili, wakati Yanga ikishinda mabao 3-0, Uwanja wa Liti, zamani ulikuwa unaitwa Namfua.

3 COMMENTS:

  1. Nyie mbona waongo waongo acheni kutuvuruga msilete chokochoko utaachaje rasilimali ukiwa unautaka ubingwa? Saleh Jembe usituvuruge

    ReplyDelete
  2. Twambie na kwa Mo wanaachwa Nani ,cse huku kwetu uhakika nilionao anankuja holding midfielder kutoka Gabon Ricardo Nzamba ,hili Mukoko asogee mbele spidi iwe zaidi ya Corona v19

    ReplyDelete
  3. Simba wanakuhusu nini?Wewe kufa na Utopolo wako.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic