JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa moja ya sehemu ambayo ataifanyia kazi kwenye usajili ni safu yake ya ushambuliaji ambayo imekuwa na mwendo wa kusuasua kwenye kutupia.
Mbali na safu ya ushambuliaji pia ameongeza kuwa ataongeza nguvu kwenye ulinzi kwa kuwa wachezaji wake waliopo bado hawajajenga nguvu zaidi anayohitaji.
"Kuna umuhimu wa kufanya maboresho ndani ya kikosi, wachezaji waliopo wanajituma na wanafanya vizuri ila kidogo inabidi tufanye maboresho ndani ya timu hasa sehemu ya ushambuliaji na ulinzi.
"Tumekuwa tukifanya makosa ya mara kwa mara jambo ambalo linatufanya tushindwe kupata matokeo, ila nina amini kwamba tutakuwa imara na tutafanya vizuri," amesema.
Ikiwa imecheza jumla ya mechi 15 imefunga mabao 9 na kuruhusu jumla ya mabao 18 ambayo wameokota Kwenye nyavu zao.
Katika mabao hayo 9, moja lilikuwa la kujifunga Kwenye mchezo wao wa Kwanza kushinda dhidi ya JKT Tanzania, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment