LICHA ya nyota wa Chelsea, Oliver Giroud kupachika bao la kuongoza dakika ya 49 kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Wolves, walikwama kulinda ushindi huo na kuyeyusha pointi tatu mazima.
Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Molineux dakika 90 zilikamilika kwa Wolves kusepa na ushindi wa mabao 2-1 ambayo yalifungwa na Daniel Podence dk 66 na lile la ushindi lilifungwa dakika za lala salama na Pedro Neto 90+5.
Chelsea ilikuwa imara ndani ya uwanja ambapo ilimiliki mpira asilimia 55 huku Wolves wakiwa na asilimia 45, mashuti walipiga jumla 13 na Wolves walipiga mashuti 12.
Pia kwa upande wa pasi, Chelsea walipiga jumla ya pasi 494 huku Wolves wakipiga jumla ya 418 ila pointi tatu zilienda kwa Wolves.
Kocha Mkuu wa Chelsea, Frank Lampard amesema kuwa matokeo hayo yamemkasirisha kwa kuwa walijipanga kupata ushindi.
"Nimekasirishwa na hili kwa kweli, tulistahili kupata ushindi ila kwa kuwa imetokea tutajipanga kwa ajili ya mechi zijazo," .
Wolves ipo nafasi ya 10 ikiwa na pointi 20 huku Chelsea ikiwa nafasi ya tano na pointi 22 zote zimecheza mechi 13.
Kitendo cha kumtoa Giroud na kumwingiza Abraham hapo ndio mchezo uliharibika. Kwa maoni yangu Abraham hana hadhi ya kuogopewa na mabeki maana hayuko agressive na ni lege lege mno
ReplyDeleteKubanwa ni kutoka sare.Kichwa cha habari kingekuwa Chelsea yachapwa na Wolves.
ReplyDeleteHawa waandishi hawa.