December 28, 2020


SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa lawama zote kuhusu uwezo wa wachezaji wake ndani ya uwanja apewe yeye na hataki kuona kwamba kuna watu ambao watawakosoa wachezaji wake.

Kocha huyo jana Desemba 27 alikiongoza kikosi chake cha Simba kushinda mabao 5-0 dhidi ya Majimaji kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho, hatua ya tatu na kutinga hatua ya nne ya mashindano hayo.


Akizungumza kwa hasira kali Vandenbroeck amesema kuwa amekuwa akiskia maneno kuhusu uwezo wa wachezaji wake pamoja na matokeo ambayo anayapata ndani ya uwanja akishinda hata akifungwa bado wanasema.

"Hatukuwa hapa nchini tulikuwa Nigeria hivi karibuni na tulishinda bao 1-0 ila watu walikuwa wanasema kuhusu wachezaji wangu pamoja na matokeo ambayo tunayapata.

“Sitaki kuona kwamba wachezaji wangu wanakosolewa kwani kwa asilimia kubwa wanajitoa na kufanya kazi kwa juhudi hilo lipo wazi.

"Haijalishi tunafungwa ama tunashinda bado hawastahili lawama iwe ni kwa mashabiki wale waliopo ndani ya timu pamoja na vyombo vya habari sitaki kuskia kuhusu wachezaji wangu wakilaumiwa nataka kulaumiwa mimi na kukosolewa iwe ni juu yangu," amesema Sven.



3 COMMENTS:

  1. Subiri safari mzee baba! Aliondoka Aussem aliyefikisha team robo final ya klabu bingwa, we ni nani?
    Your successor was fired even though he led the team to CAF quarter final, well you may survive but pray hard that you qualify to group stages.

    ReplyDelete
  2. HAIJALISHI, ANASIMAMIA ANACHOKIAMINI, KOCHA KUFUKUZWA NI KAWAIDA TU WALA HAKUNA CHA AJABU

    ReplyDelete
  3. Ndio sven waambie wasenge wasenge wasiojua mpira......... Aguero anakaa benchi huko duniani hakuna timu inayoweka fowad mbili kama kiungo kinafunga.

    Kibaden alicheza fainali ya africa lakin akafukuzwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic