December 28, 2020

 


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara ambao utakuwa ni wa raundi ya pili dhidi ya Tanzania Prisons.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Desemba 31, Uwanja wa Nelson Mandela, Rukwa.

Yanga inakutana na Prisons ikiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 kwenye mchezo wa raundi ya kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Mchezo huo langoni alikaa kipa namba mbili wa timu hiyo Faroukh Shikahlo ambaye kwa sasa amejenga ushkaji na benchi ndani ya kikosi hicho.

Ikiwa imecheza mechi 17, mechi 16 alianza Metacha Mnata ambaye ni chaguo namba moja kwa Kocha Mkuu, Cedric Kaze.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo huo na wanahitaji pointi tatu muhimu.

"Maandalizi yapo vizuri na kikosi kipo tayari kwa ajili ye mchezo wetu tunaamini kwamba utakuwa mchezo mgumu ila tunahitaji pointi tatu muhimu," .


Yanga ipo nafasi ya kwanza na kibindoni ina pointi 43 inakutana na Tanzania Prisons iliyo nafasi ya 11 na pointi 21.

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic