December 27, 2020

 


NYOTA wa zamani wa Yanga, Amiss Tambwe amesema kuwa ikiwa timu hiyo haitamlipa fedha zake za usajili pamoja na mshahara wake watajuana na Shirikisho la mpira duniani, (Fifa) kwa kuwa yeye hausiki kwenye kutoa hukumu. 


Tambwe amesema kuwa ameambiwa na mwanasheria wake kwamba kesi yake dhidi ya Yanga ameshinda hivyo kinachotakiwa ni Yanga kumlipa fedha zake anazodai.


"Mwanasheria wangu ameniambia kwamba tumeshinda kesi hivyo kinachotakiwa ni Yanga kulipa hizo fedha kama hawatalipa ni wao watajuana na Fifa mimi sijui itakuaje.


"Tulichokifanya tumewapa akaunti namba Yanga kisha tunasubiri  kuona fedha zinaingizwa. Tena zinapaswa kuingizwa zote kwa kuwa ingekuwa kidogokidogo ni wakati ule tungekubaliana ila kwa sasa hilo halipo," .

Mahakama ya Usuluhishi masuala ya michezo (CAS) imeamuru Yanga kumlipa Amisi Tambwe dola 20,000 (46.4 M Tsh) pesa ambazo alikuwa anaidai klabu hiyo kama ada ya usajili na mshahara wa miezi mitatu.

Mshambuliaji huyo aliachwa na Yanga msimu wa 2018/19 kwa kile kilichoelezwa kuwa amechukua ubora wake.


Tambwe aliondoka Yanga akiwa na madeni yake hayo ambayo klabu hiyo haikumlipa kwa wakati kiasi cha kuwashitaki CAS na chombo hicho kutoa hukumu alipwe ndani ya siku 45 kuanzia Desemba 1, 2020. 


4 COMMENTS:

  1. Ndio maana Yanga wanataka kumtapeli Morrison na simba ili wapate kulipia deni.hatari

    ReplyDelete
  2. Hii habari haivumishwi kama zile za upande mwingine. Waandishi wengi bongo wako kwenye payroll ya GSM

    ReplyDelete
  3. Hizi timu zinazingua sana mpaka wa leo Tambwe anaidai yanga licha ya wema wote aloutenda inabaoa sana

    ReplyDelete
  4. Wanapaswa kumlipa,alitumia uungwana na uvumilivu wa muda mrefu lakini walimzungusha.Wakumbuke na mema aliyoyafanya kwa klabu ya yanga.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic