CEDRIC Kaze,
Kocha Mkuu wa Yanga ana dakika 450 za moto kusaka pointi tatu muhimu ndani ya
mwezi Desemba kwa kucheza mechi tano kali kabla ya kuufunga mwaka 2020.
Kete ya
kwanza kwa Yanga itakuwa dhidi ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Mkapa Desemba 6.
Kaze atakutana na Charles Mkwasa ambaye anazijua mbinu za timu hiyo kwa kuwa
kabla ya kuibukia ndani ya Ruvu alikuwa kocha msaidizi.
Desemba
12,Yanga itawafuata Mwadui FC ambao wamekuwa na matokeo ya kusuasua ikiwa
nafasi ya 17 na pointi 10 baada ya kucheza mechi 13, Uwanja wa Kambarage
Yanga
itarejea Dar kumenyana na Dodoma, Desemba 19, Uwanja wa Mkapa itakuwa ni mara
ya kwanza kukutana ndani ya uwanja kwa kuwa timu hii imepanda daraja msimu huu.
Kaze
atakiongoza kikosi chake mbele ya Ihefu inayonolewa na Zuber Katwila, Desemba
26, Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Funga kazi
kwa 2020 itakuwa ugenini dhidi ya Tanzania Prisons ambayo iliwapa tabu watani
zao wa jadi Simba kwa kuwafunga bao 1-0 Uwanja wa Nelson Mandela itakuwa Desemba 31.
0 COMMENTS:
Post a Comment