GEORGE Lwandamina baada ya kusaini dili la mwaka mmoja ndani ya Azam FC amesema kuwa hesabu kubwa ni kufanya vizuri na atapambana kupata matokeo mbele ya Yanga na Simba.
Lwandamina raia wa Zambia aliwahi kuifundisha Yanga hivyo ana uzoefu na soka la Afrika jambo ambalo limewavutia mabosi wa Azam FC.
Akizungumza na Saleh Jembe, Lwandamina amesema kuwa anatambua ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara ni mkubwa hivyo atapambana na timu kubwa ambazo ni Yanga na Simba ili kuwapa hali ya kujiamini wachezaji.
"Najua kwamba kuna ushindani mkubwa na vita kubwa ipo kwa Simba na Yanga, nina amini kwamba tulikutana uwanjani tutapata matokeo hivyo mashabiki watupe sapoti," amesema.
Lwandamina amechukua mikoba ya Aristica Cioaba ambaye alifutwa kazi Novemba 26 ndani ya Azam FC.
0 COMMENTS:
Post a Comment