KOCHA Mkuu wa Klabu ya Yanga, Cedric
Kaze amekiri kuwa wanatarajia kuwafanyia mchujo washambuliaji wa kikosi hicho,
ili kupata watakaoweza kuwasaidia na kuwaacha wale watakaoonekana kushindwa
kuthibitisha ubora wao.
Tangu kuondoka kwa Mkongomani, Heritier Makambo, Yanga
imeonekana kuwa na hali ngumu katika safu ya ushambuliaji, ambapo kwa msimu huu
pekee mastraika wote wanne wa Yanga wamefanikiwa kufunga mabao matano pekee
kati ya 15 yaliyofungwa na timu hiyo.
Nyota hao ni pamoja na Michael Sarpong mwenye mabao matatu, Ditram Nchimbi mwenye pasi moja ya bao,Yacouba Songne mwenye bao moja na pasi mbili za mabao.
Kaze amesema: “Ni kweli
tatizo la ushambuliaji ndani ya kikosi chetu kwa sasa linaonekana kuingia
katika hatua nyingine ya kuwa tatizo sugu.
“Ukirejea michezo yetu mitatu iliyopita utagundua kuwa tulikuwa
na uwezo wa kushinda kwa mabao mengi tena dakika za mwanzo tu za michezo hiyo
lakini kwa bahati mbaya hatukufanya hivyo.
“Kwa mfano ndani ya dakika 45 tu za kwanza kwenye mchezo dhidi
ya JKT Tanzania tulikuwa tumetengeneza nafasi za wazi tatu ambazo kama
tungekuwa makini basi tungepata mabao.
“Kutokana na hali hii tumepanga kufanya tathimini ya mwenendo wa
washambuliaji wetu, ili kujiridhisha kama tunahitaji kuwapa mbinu nyingine za
ziada au tuangalie utaratibu wa kusajili mastraika wengine ambao wataweza
kuleta tofauti kwa sababu hatuwezi kuvumilia tunashinda bao moja kwenye kila
mchezo,” amesema Kaze.
Ushindi huo dhidi ya JKT umeifanya Yanga kufikisha pointi 31 na
kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi.
Mlimfukuza Kocha WA kwanza kisa mabao fukuzeni Na huyu.
ReplyDeleteAcha uzushi na kuteseka..kocha aliyefukuzwa sababu ilikuwa timu kutocheza mpira unaoeleweka na sio sababu ya kutofunga
DeleteKaze alusema alihusika katikavusajili wa wachezaji waliosajiliwa na GSM akiwepo Sarpong na Sogne. Sasa vipi tena?
ReplyDeleteHata mie nashangaa. Tuliambiwa kocha Kaze alihusika na usajili wa wachezaji wote waliosajiliwa dirisha kubwa, sasa inakuwaje tena??
DeleteTabu kwel uto
ReplyDeleteAcha ungo dogo, kazi kuvuruga timu tu😏
ReplyDeleteMwamedi fc vipi mbona mnateseka
ReplyDelete