December 22, 2020




KUNA hatihati ya nyota wawili wa kikosi cha Simba, kipa namba moja, Aishi Manula na mshambulaiji wao John Bocco wakaukosa mchezo wa kesho,  Desemba 23.

Simba itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao unatarajiwa kuchezwa kesho Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe. 

Mchezo huo utachezwa majira ya saa 9:00 alasiri kwa saa za Zimbabwe huku kwa Tanzania ikiwa ni saa 10:00 jioni.

Nyota hao wawili walipata maumivu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC ambapo Simba ilishinda bao 1-0 lilipachikwa kimiani na Meddie Kagere ambaye ametupia jumla ya mabao matano kwa msimu wa 2020/21.

Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa wachezaji hao watafanyiwa tathimini kwenye mazoezi ya leo ili kujua uwezekano wao wa kuweza kucheza kesho.


Manula alitumia jumla ya dakika 180 kwenye mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali ilikuwa mbele ya Plateau United ambapo ugenini, nchini Nigeria Simba ilishinda bao 1-0 na mchezo wa marudio uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Simba ililinda ushindi wake.

4 COMMENTS:

  1. Acha kupotosha!Walipata maumivu wapi na huku walipumzishwa na kocha??

    ReplyDelete
  2. Tatizo wabongo tunachemsha sana habari zetu na hatuogopi na ndiyo wasomaji wa magazeti cku hizi wa wachache sana..... leo unatoa habari kesho unakanusha habari hiyohiyo

    ReplyDelete
  3. Simba kila mchezaji mkali hata Kama wasipokuwepo zipo mashine mbadala nazo nhatariii, hakuna asiyemjua kagere Afrika na pia Beno ninoma.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic