December 5, 2020


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa nyota wao mpya, Saido Ntibazonkiza atafunga sana ndani ya Ligi Kuu Bara kutokana na aina ya wachezaji waliopo ndani ya timu hiyo kuwa na kasi kwenye kusaka ushindi.

Nyota huyo raia wa Burundi amesaini dili la miaka miwili kukitumikia kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa wanaamini kwa uwezo alionao nyota huyo atafunga mabao mengi.

“Mwamba Ntibazonkiza ni anajua na uwezo wake upo wazi anakutana na wachezaji wenye kujua kumtumia sasa kwa kasi yake ndani ya Yanga atafunga mabao mengi na kwa dua ambayo tumemfanyia basi atafanya makubwa.

“Kikubwa ni kuendelea kumuombea kwa Mungu ili aweze kufanya mazuri zaidi na lile tatizo la kutofunga mabao mengi litakuwa limekwisha kabisa,” amesema Nugaz.


Yanga ipo nafasi ya kwanz ikiwa na pointi 31 baada ya kucheza mechi 13, imefunga jumla ya mabao 15 kibindoni na mtupiaji wao namba moja na Michael Sarpong mwenye mabao matatu.


Mrundi huyo alitua rasmi kujiunga na kikosi Desemba 2 na kupokelewa na mashabiki pamoja na uongozi wa Yanga tayari ameshaanza mazoezi na wachezaji wenzake kambini. 

5 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic